Katika mkutano huo umeona kuwa, hivi sasa nchi za Ulaya bado zinakabiliwa na changamoto kubwa katika kutekeleza hatua za kukabiliana na msukosuko wa madeni; Marekani huenda itabana kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha; uchumi wa baadhi ya nchi za masoko mapya umeanza kuongezeka polepole, na masoko ya utoaji bidhaa kwa wingi huenda yatakabiliwa na tatizo jipya la utoaji wa bidhaa.
Mkutano huo umesema kuwa, ili kukabiliana na changamoto hizo, pande mbalimbali za kundi hilo zinapaswa kutekeleza kwa pande zote na kwa wakati ahadi husika za sera za mpango wa utekelezaji wa Los Cabos. Nchi mbalimbali zinapaswa kuhimiza mageuzi ya muundo na mambo ya fedha ili kuinua ufanisi wa uzalishaji na kuongeza ajira.